About Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Nakuru

Gardens And Parks, Urban Environment, Cultural, Interesting Places, Natural, Nature Reserves, National Parks

Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Nakuru ni mbuga ya wanyama nchini Kenya iliyoko kando ya Ziwa Nakuru, karibu na mji wa Nakuru. Umbali wa Nairobi ni km 140. Geti kuu liko kilomita 4 kutoka mji wa Nakuru. Eneo lake ni takriban km² 188. Inajulikana hasa kwa wingi wa ndege aina ya heroe na kundi la vifaru ambao wanaonekana hapa kwa uhakika mkubwa kulingana na mbuga nyingine za Kenya.

Mbuga ilianzishwa mwaka 1961. Sababu ya kuianzisha ilikuwa idadi kubwa ya ndege wa heroe wanaokusanyika hapa. Wakati mwingine huhesabiwa kuwa hadi milioni mbili. Idadi ya heroe hubadilika kimajira kulingana na kiasi cha algae ambazo ni chakula chao hasa.

Source From: Wikipedia
Nakuru, Kenya

Nearest places in Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Nakuru